TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirikishana ufahamu, uzoefu, na ujuzi katika kuendeleza na kuleta mabadiliko katika Sekta ya nzima ya Ushirika, kiuchumi na kijamii.

Akizungumza katika Kikao Kazi kilichoandaliwa  na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, leo Ijumaa Septemba 1, 2017 mjini Dodoma, Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Veneranda Mgoba amesema kazi ya uundwaji wa Majukwaa ya mikoa 16 imefanywa kwa ushirikiano wa vyama vya ushirika, wadau mbalimbali mikoani pamoja na ufadhili wa Program ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF). Kabla ya ufadhili wa MIVARF mikoa mitatu (3) ilikuwa imeunda na kufanikisha majukwaa ya kimkoa, ambayo ni Pwani, Manyara na Rukwa.

Mikoa mingine iliyounda majukwaa hadi sasa ni Mbeya, Katavi, Songwe, Kagera, Mwanza, Simiyu, Arusha, Shinyanga, Iringa, Tanga, Njombe, Lindi, Singida, Tabora, Kigoma ns Geita.

Majukwaa ya Ushirika yanalenga: kuleta uelewa kwa jamii kuhusiana na ushirika hususan vijana na wanawake; Kuweka bayana ufanisi wa ushirika miongoni mwa wanaushirika; Kupanua maeneo ya kufanyia tafiti, kutoa ushauri na kujadili changamoto zinazokabili maendeleo ya ushirika na jinsi ya kukabiliana nazo katika ngazi mbalimbali; Kuibua taasisi mpya za kiushirika kwa kuzingatia mahitaji ya wakati (mf. Ushirika wa Gesi, Uwekezaji na uanzishaji wa ushirika wa viwanda kwa kuitikia wito na utashi na kaulimbiu ya uchumi wa viwanda wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli; na Kujenga mikakati endelevu ya kuwavutia, kuwashawishi na kuwahamasisha wanachama wapya na hasa vijana kuwa wanachama wa ushirika.

Katika kiakao cha leo kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa MIVARF na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika nchini (COASCO), Taarifa kuhusu Uhakiki wa Hali ya Vyama vya Ushirika katika mikoa sita (6) iliwasilishwa na Mtakwimu Mwandamizi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Godfrey Mjatta ambayo ilionesha vyama 2,842 vilihakikiwa, ambapo vyama 1,105 (39%) vilikuwa hai, vyama 962 (34%) vilikuwa sinzia na vyama 775 (27%) havikuonekana.

Kazi ya Uhakiki wa Hali ya Vyama katika mikoa 6 ya Dodoma, Mwanza, Tabora, Mtwara, Kilimanjaro and Njombe  imefanywa na TCDC na COASCO kwa ufadhili wa MIVARF.

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top