TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa kati. Mtaka amesema  hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Simiyu uliofanyika Mjini Bariadi, tukio ambalo limeshirikisha viongozi wa Serikali na watalaam mbalimbali ngazi Mkoa huo, viongozi wa vyama vya ushirika, Tume ya Maendeleo ya Ushirika  na wadau  mbalimbali wa ushirika.

" Sisi kama mkoa tuko tayari  kwa yale ambayo  ninyi wenzetu wa Tume ya Ushirika mnadhani kupitia hayo tutakuwa na ushirika imara na utakaoendeshwa kisasa, tuko tayari hata kwa kuwatoa watu wetu kujifunza katika vyama vya ushirika vilivyofanikiwa; ushirika wa Tanzania ukiamua Uchumi wa kati inawezekana," amesema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema wananchi wakielimishwa na kukubali kuungana katika vyama ushirika wanaweza kuondokana na Umaskini,  hivyo amesisitiza uwepo wa ushirika imara wenye matokeo chanya katika maeneo muhimu ya uzalishaji, ili hata mikoa mingine ijifunze  kupitia mkoa wa Simiyu.

"Mwalimu Nyerere amewahi kusema namna pekee ya watu maskini kujikomboa ni kuungana, niwasihi wanaushirika kuunganisha nguvu katika ushirika, matajiri wanaungana kuunda makampuni yanayoweza kukopa, yakashtaki na kushtakiwa ninyi unganeni kwenye vyama vya ushirika kujenga uchumi, " amesema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) imekubali kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu kwa kuviwezesha vyama vya ushirika na vikundi vilivyosajiliwa kisheria kwa kuwajengea uwezo wanachama na kuwapa mikopo kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali, hivyo vyama vya ushirika vinapaswa kuchangamkia fursa hiyo.

Akizungumzia mchango wa ushirika katika utekelezaji wa Kauli Mbiu ya Mkoa"Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja" Mkuu huyo wa Mkoa amesema vyama vya ushirika ndivyo vyenye wazalishaji wa malighafi ya viwanda, hivyo jukwaa la ushirika litumiwe vizuri katika kuweka mikakati ya kuimarisha vyama vya ushirika na Viongozi wa Serikali wako tayari kuonesha ushirikiano.

Katika hatua nyingine Mtaka amesema mkoa unaandaa andiko linalolenga kuwakusanya wakulima na wanaushirika wote pamoja, ambapo watatumia vyumba vya madarasa katika Shule za Serikali wanafunzi watakapokuwa likizo kupewa mafunzo ya ushirika na kilimo na Wataalam wa Halmashauri, Mkoa na Chuo Kikuu cha Ushirika, ili kuimarisha ushirika na kuongeza tija katika kilimo na mifugo.

Sanjali na hilo Mtaka amesisitiza kuwa mkoa wa Simiyu ndio unaoongoza kwa kulima pamba hapa nchini, hivyo ni vema kukawa na ushirika wenye kuleta majawabu kwa changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba kuondoa kero kwa wakulima na kuongeza ubora katika uzalishaji.

Kwa Upande wake Kaimu Naibu Mrajis kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Collins Nyakunga amemshukuru Mkuu  wa Mkoa wa Simiyu kwa kuonesha nia ya kuimarisha ushirika katika mkoa huo na kuona kuwa kupitia ushirika wananchi wanyonge wanaweza kutatua matatizo yao ya kiuchumi na Kijamii.

Nyakunga amesema Tume ya Maendeleo ya Ushirika itaandaa namna ambayo itautoa ushirika katika uendeshaji wa kizamani uendeshwe kisasa, tafiti zitafanyika kupitia Chuo Kikuu cha Ushirika kuona namna ya kuongeza bei, thamani ya zao la pamba na ushirika mkoani Simiyu kuimarika.

Naye Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Simiyu, Mathias Shineneko amesema Mkoa huo umejiwekea mkakati wa kuakikisha vyama vya ushirika vinajielekeza katika kuweka taratibu za kuongeza na kuimarisha mitaji, hisa na akiba ili kujiimarisha kiuchumi.

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top