TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi vya Mazao (AMCOS) kupata bei nzuri na ya soko katika msimu huu na amezitaka AMCOS ambazo hazifanyi kazi (sinzia) ziimarishwe na kuanza kufanya kazi msimu ujao.

“Natoa rai kwa viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika kutumia fursa hii vizuri kwa kukusanya mazao kutoka kwa wakulima katika ubora unastahili na kutokujihusisha na vitendo vya ubadhirifu na wizi wa fedha za Vyama vya Ushirika,” alisema Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Tanga lililofanyika leo 27/07/2017 mjini Tanga.

Aidha, Shigela amewataka Maafisa Ushirika   wa Wilaya husika pamoja na vyombo vya usalama kufanya usimamizi wa karibu kipindi chote cha ununuzi wa mazao na kudhibiti walanguzi  binafsi wanaonunua mazao bila ya  utaratibu.

Kwa kuwa Mkoa wa Tanga unalima mazao mbalimbali, Mkuu wa Mkoa amelitaka kongamano la Wanaushirika kufikiria kuanzisha Chama Kikuu kimoja kiweze kushughulikia mazao mengine pia ili kusaidia wanaushirika katika kuwa na sauti ya pamoja na kupata bei nzuri ya mazao yao (korosho, katani, machungwa, chai na viungo).

“Katika kuelekea Uchumi wa Viwanda, Vyama vya Ushirika hususani AMCOS na Vyama Vikuu vina fursa kubwa kuchangia uchumi wa viwanda katika Mkoa wa Tanga kwani ndiyo vinategemewa kuwa wazalishaji wa malighafi za  viwanda vidogo, vya kati na viwanda vikubwa vitakavyochochea ukuaji wa uchumi, kuongeza ajira kwa  vijana na kuongeza pato  la Mkoa na Taifa,” amesema Shigela.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Jukwaa la Ushirika mkoa wa Tanga, Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Tito Haule amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika kutokutumia vyama hivyo kama vichaka vya kufanya uhalifu na akasema kuwa serikali ikiwagundua itawashughulikia kwa nguvu zake zote. Aidha, Mrajis amewataka Maafisa Ushirika kusimamia vyama vya ushirika kwa ueledi, uaminifu na uadilifu ili vyama hivyo viendeshwe kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

 Akisoma Taarifa ya Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Tanga, Majis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa  wa Tanga, Jackline Senzighe amesema kuwa Mkoa wa Tanga una Vyama vya  Ushirika 387; mazao (71), Akiba na Mikopo - SACCOS (232),  mifugo (32) umwagiliaji (11), madini (6), uvuvi (4), ufundi (9), michepuo mingine 20 na vyama vikuu (2); ambapo vyama hivyo vina jumla ya wanachama 46,687.

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top