TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo hiyo imeongezeka kutoka shilingi billion 4.5  iliyotolewa Mwaka 2005.

Taarifa ya Maendeleo ya Shughuli za Ushirika Mkoa wa Arusha iliyotolewa na Majis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Arusha, Emmanuel Sanka katika Ufunguzi wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Arusha lililofanyika leo 25/07/2017 mjini Arusha imebainisha kuwa idadi ya SACCOS zilizosajiliwa imeongezeka na kufikia 371 Juni, 2017 kutoka 94 mwaka 2005.

Sanka amesema idadi ya wanachama  katika SACCOS imeongezeka kutoka 9,326 mwaka 2005 hadi  50,689 Juni 2017 . Hisa, Akiba na Amana imeongezeka toka shilingi bilioni 3.8 mwaka 2005 hadi shilingi bilioni 40 Juni, 2017. 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Arusha amewataka Viongozi na Watendaji  wa  Vyama vyote vya Ushirika mkoa wa Arusha wahakikishe kuwa  Vyama vya Ushirika vinasimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa  Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya Mwaka 2013 na Kanuni zake na Masharti yaliyowekwa.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi kujiepusha na  vitendo viovu kama vile  ubadhirifu/wizi, matumizi mabaya ya madaraka, viongozi kujikopesha mikopo mikubwa hali inayowafanya kushindwa kulipa madeni, kutokuwajibika na uzembe, ambapo vitendo hivi vinasababisha Vyama vya Ushirika  kuendelea kuzorota na kushindwa kutoa huduma kama ilivyotarajiwa.

Akitoa Maelezo ya Awali ya  Jukwaa, Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Tito Haule amesema kuwa Wanaushirika wayatumie Majukwaa ya Ushirika kujadili Maendeleo na  Changamototo zinazojitokeza katika Sekta ya Ushirika na kutoa mapendekezo ya namna ya kuzitatua changamoto hizo. Aidha, Mrajis amewataka viongozi wa Vyama vya Ushirika nchini kuwa Waaminifu na Waadilifu kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitawafumbia macho Wabadhilifu wa Mali katika Vyama vya Ushirika na kazi ya kuwaondoa Viongozi wanaokiuka maadili ya kazi zao imeanza.

Mkoa wa Arusha una Vyama vya Msingi 496  na Chama Kikuu 1. Kwa kulinganisha na idadi ya vyama 174 vilivyokuwepo mwaka 2005, hivyo kuwa na ongezeko la vyama 290 sawa na asilimia 162. Kati ya vyama hivyo vya Msingi; 371 ni Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), 54 AMCOS, 17 Vyama vya walaji, vyama 13 vyama vya Viwanda, 27 vyama vya mifugo, 6 vyama vya huduma, 3 vyama vya umwagiliaji, na 2 vyama vya wakulima wa mboga, 1 cha madini, 1 wauza vinyago na 1 cha usafirishaji. Idadi ya wanachama wa vyama hivyo imeongezeka toka 36,000 mwaka 2005 hadi 70,320 (asilimia 95) mwaka 2017; ikiwa wanaume ni 23,796 na wanawake 32,535  na mtaji wa vyama hivyo umeongezeka toka shs bilioni 4 hadi shs bilioni 40 (asilimia 675).

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top