TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi usiku na mchana ili Kumaliza Migogoro ya Kiushirika katika maeneo yao na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa katika kuongeza kipato kwa Wanaushirika.

“Nawataka muende mkachape kazi kama mchwa, usiku na mchana bila kulala tuweze kumaliza viporo vilivyopo vya migogoro ya kiushirika katika maeneo yenu, ili tuweze kupata nafasi ya kuanza mambo mapya ya kuijenga Sekta ya Ushirika,” amesema Ole Nasha.

Waziri Ole Nasha ametoa wito huo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika ulioanza leo Mei 30, 2017 mjini Dodoma ambapo pia amewataka kubuni mikakati mipya ya uendeshaji wa vyama na kuondokana na utegemezi wa mikopo na kujenga uwezo wa kimtaji ndani ya vyama, kuanzisha mifumo mipya ya masoko ikiwemo stakabadhi ya mazao ghalani, commodity exchange market na kuongeza thamani mazao kabla ya kuyauza.

Waziri Ole Nasha amesema usimamizi wa Vyama vya Ushirika nchini umekuwa dhaifu kutokana na kutowajibika kwa baadhi ya Warajis Wasidizi wa mikoa ambapo kumesababisha mamlaka za juu zaidi kuchukua hatua dhidi ya viongozi wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu kwenye Vyama vya Ushirika. Mfano hatua zilizochukuliwa katika Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku wa Kanda ya Magharibi WETCU Ltd na Nyanza Cooperative Union.

“Kiuhalisia hata ninyi Warajisi Wasaidizi wa Mikoa hiyo mlihitaji kuwajibishwa kwa namna moja au nyingine. Wajibikeni na msisubiri uongozi wa juu uje kuwasaidia kazi zenu. Baada ya mkutano huu wa leo wa kujitafakari itabidi kila Mrajisi abebe mzigo wake,” amesema Naibu Waziri.

Waziri Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa kufanya mambo yafuatayo: kubadilika na kuwa na mtizamo mpya na dhamira mpya ya uendeshaji na usimamizi wa Vyama vya Ushirika; kusimamia Vyama vya Ushirika kwa karibu ili vifanye shughuli zake kwa ufanisi badala ya kusubiri mambo yaharibike, kutokusubiri wizi na ubadhirifu utokee ndipo muende kufanya uchunguzi; kuwa na upeo wa hali ya juu wa kuweza kutoa ushauri wa kitaalamu (technical backstopping) kwa Vyama vya Ushirika hususani kwenye maeneo ya menejimenti ya fedha na Mikopo, masoko, uwekezaji, makisio ya mapato na matumizi na ukomo wa madeni; kufanya usimamizi madhubuti wa utendaji na maadili ya Maafisa Ushirika kwenye maeneo yenu; kufanya kazi kwa kuzingatia matokeo ya kazi (Results Oriented); na kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uaminifu.

Waziri Ole Nasha amemtaka Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Bw. Tito Haule kuanzia sasa kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuwashusha vyeo na mishahara Warajis Wasaidizi wa Mikoa watakaoshindwa kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha, Naibu Waziri amesema kuwa Serikali haitawaacha kwenye nafasi za uongozi Warajis Wasaidizi kama masuala mapya yafuatayo yataendelea kujitokeza kwenye maeneo yao: Wizi na ubadhirifu utakayojitokeza kuanzia sasa kwenye Vyama vya Ushirika; Maafisa Ushirika watakaobainika kwenye maeneo yao kutotimiza wajibu ipasavyo wa usimamizi wa Vyama vya Ushirika na kujihusisha na wizi, ubadhirifu na rushwa; Vyama vya Ushirika kuchukua mikopo na kuwekeza kwenye maeneo yasiyo na tija na hivyo kusababisha mali za wanaushirika kuuzwa; Kutofanyika kwa uhamasishaji na hivyo kupungua kwa idadi ya Vyama vya Ushirika na wanaushirika; Kutowachukulia hatua Maafisa Ushirika wazembe, wasio wajibika, wala rushwa na wanaoshirikiana na baadhi ya viongozi wa Vyama kuhujumu au kufanya ubadhirifu wa rasilimali za ushirika; na kukosekana kwa Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za vyama ikiwemo ubabe na ukiukaji wa sheria katika kuendesha mikutano mikuu.

Latest News

Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi usiku na mchana ili Kumaliza Migogoro ya Kiushirika katika maeneo yao na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa katika kuongeza kipato kwa Wanaushirika.  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum iliyoitishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini. Vyama 135 Bodi zake zimevunjwa katika mkoa wa Mtwara na vyama 55 Bodi zake zimevunjwa katika mko [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa kifungu cha 126 cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 kutokana na makosa mbalimbali yaliyobainishwa katika  uchunguzi juu ya uendeshaj [ ... ]

Read more
Msikimbilie Mikopo isiyokuwa na Tija – MrajisMsikimbilie Mikopo isiyokuwa na Tija – Mrajis
06 Apr 2017 12:52

  Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Tito Haule amevitaka Vyama vya Ushirika nchini kujiepusha kujiingiza kwenye mikopo isiyokuwa na tija kutoka katika taasisi za kifedha, ambayo inavigharimu vyama hivyo na kushindwa kujiendesha kutokana na kuzidiwa na madeni ambayo hayaendani na uwezo hali [ ... ]

Read more
Nishati Mbadala ya Kukausha Tumbaku Nishati Mbadala ya Kukausha Tumbaku
06 Apr 2017 12:43

  Katika kukabiliana na baadhi ya changamoto za uharibifu wa mazingira na utunzaji wa miti katika uzalishaji na ukaushaji wa tumbaku, Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited (PATL) imekuja na Mradi wa Nishati Mbadala ya kuni ambayo ni nyasi aina ya magugu (Elephant grass). Kampuni ya Premium A [ ... ]

Read more
Bodi ya SACCOS ya Walimu Ulanga yawajibishwaBodi ya SACCOS ya Walimu Ulanga yawajibishwa
03 Apr 2017 11:26

Bodi ya Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Walimu Wilaya ya Ulanga (Ulanga Teachers Savings & Credit Co-operative Society Ltd) imewajibishwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutumia fedha za Mkopo toka Benki ya CRDB kiasi cha Shilingi 258,424,920/= kinyume na makusudio ya mkopo na kughush [ ... ]

Read more
Kuondolewa Madarakani kwa Bodi za Ayalabe Kuondolewa Madarakani kwa Bodi za Ayalabe
24 Mar 2017 08:33

Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania  (Tanzania Cooperative Development Commission- TCDC) kwa kuzingatia Sheria ya vyama vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013 na taaarifa ukaguzi na uchunguzi imeamua kuziondoa madarakani Bodi ya Ayalabe SACCOS Ltd  na Bodi ya Ayalabe Dairy Cooper [ ... ]

Read more
Wabadhirifu katika Vyama vya Ushirika WadhibitiweWabadhirifu katika Vyama vya Ushirika Wadhibitiwe
24 Mar 2017 06:19

  Ushirika ni dhana muhimu inayowasaidia Wananchi hasa wenye kipato cha chini na kati kuanzisha na kumiliki chombo chao (chama cha ushirika) kidemokrasia na kuchangia mtaji unaohitajika kwa usawa na kukubali kuyakabili matatizo na kupata manufaa kutokana na shughuli za chombo hicho ambazo wao hush [ ... ]

Read more
Other News 

Online Users

We have 28 guests and no members online

Go to Top