TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum iliyoitishwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini. Vyama 135 Bodi zake zimevunjwa katika mkoa wa Mtwara na vyama 55 Bodi zake zimevunjwa katika mkoa wa Lindi.

 Akiongea na Waandishi wa Habari mkoani Mtwara leo Mei 9, 2017 Kaimu Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Augustino Semkuruto amesema Bodi za Uongozi wa AMCOS katika Mkoa wa  Mtwara na Lindi  zimevunjwa baada ya kusomewa Taarifa za Ukaguzi wa Hesabu za Vyama hivyo katika  mwaka wa fedha 2015/2016 ambayo ilionyeha dosari mbalimbali, hususan matumizi mabaya ya fedha za Vyama.

 Wilaya na idadi ya Vyama ambavyo Bodi zake zimevunjwa katika mkoa wa Mtwara, Chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2015 ni Tandahimba (67), Newala (!5), Nanyumbu (16), Maasi (23), Mtwara Vijijini (7), Mtwara Manispaa (1) na Nanyamba (6).

 Wilaya na idadi ya Vyama ambavyo Bodi zake zimevunjwa katika mkoa wa Lindi ni Ruangwa (11), Nachingwea (16), Lindi Vijijini (9), Liwale (12), Kilwa (6) na Lindi Manispaa (1). Mwaka 2017 ni Mwaka wa Uchaguzi wa Viongozi wa Bodi za Vyama vya Ushirika kwa awamu ya pili baada ya Uchaguzi wa awamu ya kwanza uliofanyika mwaka 2014, chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya Mwaka 2013.

 Kwa kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi; Semkuruto amewahimiza wanachama wa vyama vya ushirika kote nchini  kuchukua fomu za kugombea uongozi katika ngazi Mbalimbali za Vyama vya Ushirika.  Kuanzia ngazi ya Vyama vya Ushirika Vya Msingi, AMCOS, Vyama  vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCOS), Vyama vya Msingi vya aina nyingine, Vyama Vikuu  na Baadae Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini.

Latest News

Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Msikimbilie Mikopo isiyokuwa na Tija – MrajisMsikimbilie Mikopo isiyokuwa na Tija – Mrajis
06 Apr 2017 12:52

  Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Tito Haule amevitaka Vyama vya Ushirika nchini kujiepusha kujiingiza kwenye mikopo isiyokuwa na tija kut [ ... ]

Read more
Nishati Mbadala ya Kukausha Tumbaku Nishati Mbadala ya Kukausha Tumbaku
06 Apr 2017 12:43

  Katika kukabiliana na baadhi ya changamoto za uharibifu wa mazingira na utunzaji wa miti katika uzalishaji na ukaushaji wa tumbaku, Kampuni ya Pre [ ... ]

Read more
Bodi ya SACCOS ya Walimu Ulanga yawajibishwaBodi ya SACCOS ya Walimu Ulanga yawajibishwa
03 Apr 2017 11:26

Bodi ya Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Walimu Wilaya ya Ulanga (Ulanga Teachers Savings & Credit Co-operative Society Ltd) imewajibi [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top