TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

 

Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa kifungu cha 126 cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 kutokana na makosa mbalimbali yaliyobainishwa katika  uchunguzi juu ya uendeshaji wa shughuli za Shirikisho hilo uliofanywa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika. 

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo Ushirika nchini, Tito Haule, kwa mamlaka aliyopewa kisheria ameiondoa Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika – TFC katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo uliofanyika Alhamisi, tarehe 13 Aprili, 2017 mjini Dodoma.

Akizungumza katika Mkutano huo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika mkutano huo, amewataka Wanaushirika kote nchini kuisoma, kuielewa na kuitekeleza kwa usahihi Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya Mwaka 2013 ambayo ndiyo inayoainisha uendeshaji wa Sekta ya Ushirika hivi sasa.

Aidha, Dkt. Tizeba amemtaka Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kutumia mamlaka aliyopewa kisheria kuhakikisha maslahi ya wanaushirika yanalindwa na kuwanufaisha wananchi hao badala ya kuwaachia viongozi wa vyama kujinufaisha wenyewe kutokana na mali zinazopatikana katika vyama hivyo.

Akisoma Taarifa ya Uchunguzi uliofanywa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Kaimu Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika, Revocatus Nyagilo,  alizitaja baadhi ya tuhuma zilizobainishwa katika uchunguzi huo ni pamoja na: Mchakato wa uuzwaji wa nyumba za Shirikisho kutokuwa wazi na bila kuwepo kwa Maazimio ya Mkutano Mkuu, matumizi mabaya ya fedha za mauzo ya nyumba kiasi cha Shilingi milioni 880, kununua gari (Toyota Prado) kinyume na utaratibu na matumizi mabaya ya fedha za chama Shilingi bilioni 3 ikiwa ni malipo ya ziada kwa Mkandarasi wa jengo la Ushirika Towers.

Kutokana na kuondolewa madarkani kwa Bodi, Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliunda Bodi ya Mpito ili kusimamia uendeshaji wa Shirikisho hilo kwa muda

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top