TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

 

Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Tito Haule amevitaka Vyama vya Ushirika nchini kujiepusha kujiingiza kwenye mikopo isiyokuwa na tija kutoka katika taasisi za kifedha, ambayo inavigharimu vyama hivyo na kushindwa kujiendesha kutokana na kuzidiwa na madeni ambayo hayaendani na uwezo halisi wa vyama husika. Madeni hayo huwaingiza wanachama wao katika matatizo kutokana na kushindwa kulipa madeni hayo. Amewashauri kuangalia huduma ambazo zinawalenga wanachama moja kwa moja.

 Mrajis ameyasema hayo Machi 30, 2017 mjini Dodoma wakati wa kusaini makubaliano na Benki ya Wanawake ya Covenant ambayo yataiwezesha benki hiyo kuweza kutoa huduma mbalimbali za bima pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kwa vyama vya ushirika nchini.  

 Bw. Haule ameitaka benki hiyo kuhakikisha inatimiza adhma ya kutoa huduma ambazo zitawanufaisha wanachama moja kwa moja na sio viongozi wachache.

"Vyama vingi vimekuwa na mazoea ya kujiingiza katika mikopo mikubwa na wakati mwingine hata kuzidi uwezo halisi wa vyama husika, lakini pia viongozi wanaokuwepo wanakuwa sio waaminifu na kujikuta wanashindwa kusimami matumizi ya fedha hizo kwa uaminifu na kujikuta wanaviingiza vyama katika matatizo makubwa,” alisema Haule.

  “Ninawsaihi viongozi waache utaratibu huu ambao umeendelea kuvifanya vyama vya ushirika kushindwa kuwa sehemu ya ukombozi wa wanachama wake bali sehemu ya kuwakandamiza,” alisema Mrajis.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, amesema atahakikisha benki yake inafanya kazi waliyokubaliana na Mrajis, ambaye ni msimamizi wa vyama vya ushirika kwa uaminifu na weledi ili kuweza kuwainua wanachama wa vyama vya Ushirika.

“Tumefanya utafiti kwa muda mrefu sasa, kuangalia namna ambavyo tunaweza kuwasaidia wajasiriamaliwadogo miongoni mwao wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na wafanya biashara, tumegundua wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo kukosa huduma za Bima ya matibabu pamoja na ajali, hivyo tumeanzisha huduma hizo ili kuwaondolea mzigo ambao wanaupata kila siku wanapopata fedha wanashindwa kuweka akiba,” alisema Mwanbenja.

 

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top