TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

 

Katika kukabiliana na baadhi ya changamoto za uharibifu wa mazingira na utunzaji wa miti katika uzalishaji na ukaushaji wa tumbaku, Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited (PATL) imekuja na Mradi wa Nishati Mbadala ya kuni ambayo ni nyasi aina ya magugu (Elephant grass).

Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited inatumia teknolojia ya Nishati Mbadala mkoani Mbeya katika wilaya ya Chunya ambapo kampuni hiyo imelima mashamba ya nyasi aina ya magugu (Elephant grass) na inayachakata majani hayo na kupata kuni (Briquettes /vitofali) za kukaushia tumbaku. Kuna aina mbili za nyasi (Elephant Grass) ambazo zinapandwa, kukuzwa na kuchakatwa ili kupata vitofali  vinavyotumika katika kukaushia tumbaku: Miscanthus Sinensis na Miscanthus Giganteus.

Faida ya Nishati ya kutumia vitofali (Briquette) vilivyotengenezwa kwa kutumia Elephant Grass (nyasi) ni nafuu kupatikana, inatoa kiwango kikubwa cha joto, inalinda miti kwa kuwa watu hawatokata miti kama kuni, rafiki kwa mazingira na ni ya muda mrefu  na vilevile inatoa ajira kwa wanajamii.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bwana Tito Haule alipotembelea kampuni ya   Premium Active Tanzania Limited hivi karibuni amevitaka Vyama vya Ushirika na wakulima kote nchini kuongeza juhudi katika kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya tumbaku nchini na duniani kwa ujumla ikiwemo uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji miti ya kukaushia tumbaku. Katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira, Bw. Haule amewataka wakulima wa tumbaku kutumia teknolojia ya Nishati Mbadala ya Kukausha Tumbaku inayotumiwa na Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited badala ya kuendelea kutumia kuni ambazo ni shida kupatikana na ukataji wa miti unsababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo kusababisha jangwa.

Bwana Haule alitoa ushauri huo wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Mbeya aliyoifanya mwanzoni mwa mwezi Machi, 2017 ambapo alitembelea kiwanda cha uzalishaji wa kuni/vitofali vya kukaushia tumbaku (Briquette Factory), alifungua maghala yaliyojengwa na Vyama vya Msingi {AMCOS} za Kalangali, Igangwe, Majengo na Mtande wilayani Chunya na alikuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa Mkuu wa 17 wa kawaida wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Chunya (CHUTCU LTD). 

“Naipongeza Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited (PATL) kwa kubuni na kuanzisha mradi wa mashamba ya nishati mbadala ya kuni ambayo ni nyasi aina ya magugu (Elephant grass). Nawashauri wakulima wa tumbaku muitumie tekinolojia hii kwa kuanzisha mashamba ya namna hiyo ili kuondokana au kupunguza gharama ya kupanda miti kila mwaka. Nimeambiwa majani hayo ukipanda yanachukua mwaka mmoja na kuanza kutumika, tofauti  na miti ambayo inachukua miaka 5 hadi 10 ili iweze kuanza kutumika. Nimeambiwa pia majani hayo ukipanda unaweza kuvuna kwa miaka kumi  mfululizo ili mradi mifugo wasiingie na kuharibu,” alisema Bw. Haule.

Meneja Mradi wa Nishati Mbadala ya Kukausha Tumbaku wa Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited Fredy Essau anasema kazi ya kulima mashamba ya nyasi aina ya magugu (Elephant grass) inaanza  kwa Uchaguzi wa Ardhi ambapo mkulima anatakiwa kuandaa eneo na kuhakikisha kuwa hakuna miti asilia ambayo itaharibiwa katika hatua hiyo.

“Kwamujibu wa taratibu nzuri za kilimo (GAP), asilimia kumi (10%) ya uoto wa asili inatakiwa kubakishwa na maeneo muhimu ya kimazingira hayatakiwi kufyekwa,” anasema Essau.

Mkulima anapochagua shamba la kulima nyasi anatakiwa kuepuka ardhi iliyokufa/ardhi isiyofaa/ iliyoachwa kwa uzalishaji wa mazao na anatakiwa asikate miti wakati wa kufungua ardhi. Aidha, mkulima anatakiwa kuandaa ardhi kipindi ambacho anaandaa mashamba ya tumbaku.

Bwana Essau anasema vipimo vya upandaji wa magugu (Elephant grass) vinavyotakiwa ni kwa kuacha nafasi (spacing), mstari kwa mstari sentimita 100 na nafasi kati ya mche kwa mche ni sentimita 50. Mbolea inayotakiwa kutumika wakati wa kupanda ni gram 10 za Double Ammonium Phosphate (DAP) na Top Dressed: gram 10 ya Urea. Aidha, jivu toka kwenye bani laweza  kutumika wakati wa upandaji miche.

Kuna njia mbili za upandaji wa magugu (Elephant grass); Upandaji wa kufukia (zamisha) na Upandaji wa njia ya Mambo. Hata hivyo, upandaji kwa njia ya kufukia (laid planting) inapendekezwa zaidi na inategemewa kuota baada ya siku kumi (10). Aina ya Elephant Grass inayopendekezwa ni Miscanthus Giganteus ambayo inatoa mavuno mengi na miche yake inapatikana kwa urahisi na vilevile ina asili ya Tanzania.

Elephant Grass (nyasi) zikiingizwa kwenye mashine na kukatwa vipande vidogo vidogo kabla ya kuingizwa kwenye Mashine ya kutengeneza Vitofali (Briquetting Machine).

Wastani wa uzalishaji wa nyasi kwa ekari  mbili na nusu (2.5) ni kilo 25,000 – 35,000. Wastani huu ni kwa Nyasi aina ya Giganteus. Wastani wa uzalishaji wa tumbaku kwa  ekari mbili na nusu (2.5) ni kilo  1,580, makisio ya vitofali kukausha Hekta moja ya tumbaku  ni kilo 5,000 na wastani wa uzito wa kitofali kimoja ni kilo 0.8.

Jiko lenye mlango linatumika kuchoma vitofali, Kilo 490 za vitofali hutumika

Kiwango cha joto cha Elephant Grass kwa mujibu wa utafiti ni 4.5kWh/Kg na kiwango cha unyevu nyevu  ni asilimia 10-12. Ukilinganisha na kiwango cha joto cha kuni mbichi 2.3kWh/Kg na takriban unyevu nyevu wake ni asilimia 50. Kiwango cha joto cha kuni kavu ni 4.0kWh/Kg na takribani unyevu nyevu  wake ni  asilimia 20.

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top