TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania  (Tanzania Cooperative Development Commission- TCDC) kwa kuzingatia Sheria ya vyama vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013 na taaarifa ukaguzi na uchunguzi imeamua kuziondoa madarakani Bodi ya Ayalabe SACCOS Ltd  na Bodi ya Ayalabe Dairy Cooperative Society Ltd  baada ya Tume kubaini ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka yaliyofanywa na bodi hizo. Vyama hivi vipo katika Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.  Hali hiyo ya uendeshaji mbovu imepelekea vyama kuwa na migogoro isiyoisha kwa takribani miaka mitatu (3)

Baadhi ya tuhuma zinawahusu wajumbe wa Bodi hizo ni pamoja na kuingia mikataba isiyo na tija pasipo idhini ya Mrajis kinyume na Sheria ya vyama vya ushirika ya 2013, Kutoandaa hesabu za vyama kwa ajili ya ukaguzi, kufanya matumizi yasio na makisio yaliyoidhinishwa na Mrajis kinyume na Sheria ya vyama vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013.

Kutokana na kuondolewa kwa Bodi hizo, Tume ya Maendeleo ya Ushirika itasimamia kwa muda uendeshaji wa shughuli zote za vyama hivyo ikiwemo kusimamia ulipaji wa mkopo toka taasisi za fedha na Serikali,  na kuhuisha shughuli  za kiwanda cha usindikaji wa maziwa.

Tume itatoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ikiwemo Ofisi ya Usalama wa Taifa, Polisi na TAKUKURU ambavyo vinaendelea na uchunguzi wa tuhuma zilizopo kwa lengo la kuwachukuliwa hatua wale wote watakaothibitika.

 Aidha, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa ubadhirifu wa fedha za chama baada ya kukamilika kwa taratibu za uchunguzi. Watuhumiwa wa ubadhirifu huo ni pamoja na Wajumbe wa Bodi zilizoondolewa, Watumishi wa Tume wanaohusika; na Kampuni au watu wote wanaotuhumiwa kuhusika katika kuhujumu vyama hivyo vya ushirika.

Tume itaitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama mara baada ya uteuzi wa Bodi za Mpito kwa lengo la wanachama kuidhinisha Bodi hiyo na Kupata taarifa ya hatua zilizochukuliwa.

 Natoa wito kwa viongozi wa vyama vya ushirika na wasimamizi wa ushirika kote nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kusimamia misingi ya ushirika kama ilivyoelekezwa katika Sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013.  Tume itaendelea kuboresha usimamizi wa vyama vya ushirika kwa lengo la kudhibiti wizi, ubadhilifu na matumizi mabaya ya ofisi yanayofanywa na baadhi ya watendaji, viongozi wa vyama vya ushirika na watendaji wa Tume nchini.  Aidha Tume haitasita kuchukua hatua kali za kisheria na kiutawala kwa wale wote watakaobainika kufanya wizi, ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka. 

 

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top