TITO HAULE

REGISTRAR OF COOPERATIVE SOCIETIES

 

Ushirika ni dhana muhimu inayowasaidia Wananchi hasa wenye kipato cha chini na kati kuanzisha na kumiliki chombo chao (chama cha ushirika) kidemokrasia na kuchangia mtaji unaohitajika kwa usawa na kukubali kuyakabili matatizo na kupata manufaa kutokana na shughuli za chombo hicho ambazo wao hushiriki kikamilifu. Ushirika pia unatoa fursa kwa wananchi hasa wenye uwezo mdogo kuunganisha nguvu zao pamoja katika kujijengea nguvu za kiuchumi ambazo ni muhimu katika kukabiliana na ushindani wa soko huru na utandawazi. Katika Vyama vya Ushirika, wanachama wana jukumu la kutatua matatizo yao ya kiuchumi na kijamii kwa kutumia juhudi zao za pamoja katika kufikia malengo ambayo yasingefikiwa kwa juhudi za mtu mmoja mmoja.  Ndiyo maana Wahenga walisema; “Umoja ni Nguvu, Utengano ni Udhaifu”. Nguvu ya Wakulima Wadogo, Wafugaji, Wavuvi, wafanyabiashara nakatika nyanja nyingine zote ipo kwenye Umoja na Mshikamano ambavyo huzaa USHIRIKA.

Pamoja na umuhimu wa Ushirika, baadhi ya viongozi katika vyama hivyo hutumia mamlaka waliyopewa kujinufaisha na kuwanyonya wanachama. Serikali imekuwa ikiwachukulia hatua kali viongozi na watendaji hao kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika ya Mwaka 2013 na sheria nyinginezo za nchi mara tu wanapotumia vibaya madaraka yao Serikali imekuwa ikiwachukulia hatua kali viongozi na watendaji hao kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika ya Mwaka 2013 na sheria nyinginezo za nchi mara tu wanapotumia vibaya madaraka yao. Hata hivyo, jitihada hizo peke yake hazitaweza kumaliza matatizo ya wanaushirika hasa wakulima ikiwa wanchama wenyewe hawachukui hatua zozote kulinda na kusimamia maslahi na biashara ya vyama vyao.

Mathalani, kilichotokea mkoani Mtwara katika mwaka msimu wa korosho wa 2015/2016 ni mfano dhahiri wa matatizo sugu ya uongozi na usimamizi katika vyama vya ushirika nchini. Matatizo ya uongozi na usimamizi dhaifu wa ushirika mkoani Mtwara umesababisha uhai wa baadhi ya Vyama vya Ushirika vya Mazao na Masoko (AMCOS) za mkoa huo kuwa mashakani. Hilo linatokana na AMCOS hizo kuwa na baadhi ya Viongozi pamoja na Watendaji wasiokuwa waaminifu. Hali hii imepelekea baadhi ya wanachama kushindwa kupata stahiki zao kila msimu ikiwa ni pamoja na kubebeshwa mizigo ya madeni wasiyostahili kuibeba wakati hali zao kifedha zikizidi kudidimia sanjari na uhai wa AMCOS zao kutia mashaka.

Kupitia Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) Serikali ilifanya ukaguzi wa hesabu za AMCOS zilizopo katika Wilaya za Mkoa wa Mtwara kwa msimu wa mwaka 2015/2016 ulioishia tarehe 30 Aprili, 2016. Ukaguzi huo ulifanyika kutokana na malalamiko yaliyotolewa na wakulima ya kufanyika kwa ubadhirifu katika AMCOS ambazo wao ni wanachama. Taarifa ya COASCO ilionyesha matatizo mbalimbali ya kiutendaji, usimamizi na ubadhirifu katika AMCOS za mkoani Mtwara. Matatizo yaliyojitokeza yalitakiwa kufanyiwa kazi na Mrajis wa Vyama vya Ushirika kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013. 

Ili kufanikisha kazi ya kushughulikia matatizo ya vyama vya ushirika mkoani Mtwara, hasa AMCOS, Tume ya Maendeleo ya Ushirika ilizikutanisha Mamlaka za Kiserikali kwa maana ya Serikali katika ngazi ya Mkoa, Serikali katika ngazi za Wilaya na Halmashauri za Mkoa wa Mtwara, Wabunge, COASCO, Bodi ya Korosho pamoja na Tume yenyewe ili kuweza kufanya Kikao cha Pamoja kwa lengo la kujadili matokeo ya taarifa ya ukaguzi wa AMCOS. Mrajis wa Vyama vya Ushirika alitumia kikao hicho kuweka wazi hatua anazokusudia kuzichukua kwa wahusika wote wa ubadhirifu katika vyama hivyokama taarifa ya ukaguzi wa COASCO inavyoeleza.

 

Wajumbe wa kikao hicho walikubaliana kuwa hatua za haraka zichukuliwe kwa viongozi na watendaji wa vyama hivyo waliohusika katika kuzorotesha maendeleo ya ushirika mkoani humo na kunusuru AMCOS za mkoa huo na kuondoa dhuluma ilyofanywa kwa wakulima wa korosho kwa mwaka 2015/2016. Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bwana Tito Haule alisema kuwa Serikali itachukua hatua na maamuzi ya haraka kwa kuitisha

Latest News

Makamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwaMakamu Mwenyekiti wa Tume achaguliwa
14 Sep 2017 16:39

  Kikao cha kwanza cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kimemchagua Bibi. Elizabeth C. Makwabe kuwa Makamu mwenyekiti wa Tume ya Maendele [ ... ]

Read more
Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Ushirika
04 Sep 2017 05:22

Mikoa 19 imeanzisha Majukwaa ya Uhirika nchini yenye lengo la Kuwakutanisha wanaushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika kwa madhumuni ya kushirik [ ... ]

Read more
Viongozi wa SCCULT wasimamishwaViongozi wa SCCULT wasimamishwa
24 Aug 2017 07:52

Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama wa SCCULT Ltd Umewasimamisha Uongozi Watendaji na Menejimenti ya SCCULT ili Kupisha Uchunguzi Utakaofanywa na Serik [ ... ]

Read more
Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)Wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
16 Aug 2017 11:46

Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya [ ... ]

Read more
Simiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC MtakaSimiyu Inahitaji Ushirika Imara – RC Mtaka
07 Aug 2017 09:06

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  amesema Mkoa wa Simiyu unahitaji ushirika imara na wa kisasa unaolenga kuwafikisha wananchi katika Uchumi wa [ ... ]

Read more
 Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia Wanaushirika kupata bei nzuri, Tanga
28 Jul 2017 15:05

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani (Stakabadhi Mazao Ghalani) umewezesha Vyama vya Ushirika vya msingi  [ ... ]

Read more
Wanaushirika wakopeshana Bilioni 230, ArushaWanaushirika wakopeshana Bilioni 230, Arusha
26 Jul 2017 13:50

Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) mkoani Arusha vimewakopesha wanachama wake Shilingi billion 230  kufikia Juni, 2017, ambapo mikopo h [ ... ]

Read more
Waziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika NchiniWaziri Mkuu atoa maelekezo kuimarisha Ushirika Nchini
02 Jul 2017 18:46

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa maelekezo  kwa Mamlaka na Taasisi za Serikali ya kuimarisha Sekta ya Us [ ... ]

Read more
 Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika Waziri aagiza TFC Kusimamia mipango ya maendeleo ya Vyama vya Ushirika
02 Jul 2017 17:15

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha, ameagiza Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini (Tanzania Federation of Coopera [ ... ]

Read more
Warajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kaziWarajis wa Ushirika watakiwa kuchapa kazi
05 Jun 2017 11:38

Naibu Waziri Wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa wa Vyama Vya Ushirika nchini kufanya kazi  [ ... ]

Read more
Bodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwaBodi za Uongozi wa AMCOS 190 zavunjwa
23 May 2017 05:33

Bodi za Uongozi katika Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 190 zimevunjwa katika mikoa ya  Mtwara na Lindi kwenye Mikutano Mikuu Maalum [ ... ]

Read more
Bodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakaniBodi na Menejimenti ya TFC waondolewa madarakani
18 Apr 2017 05:08

  Bodi ya Uongozi pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC Ltd) imeondolewa madarakani na kuwajibishwa kwa mujibu wa  [ ... ]

Read more
Other News

Go to Top